Tuesday, June 3, 2014

Maskini wafanyabiashara wa kituo cha mwenge




WAFANYABIASHARA wa eneo la Kituo cha Daladala Mwenge, Dar es Salaam, wameilalamikia serikali kwa kuhamisha kituo hicho na kukipeleka Makumbusho kwa kuwa sasa biashara zao zimedorora.
“Kwenye mkusanyiko wa watu siku zote biashara inafanyika, lakini baada ya kufungwa kwa huduma za daladala biashara zetu haziendi, na maeneo ya biashara tumeshayalipia, hivyo hatuwezi kuhama,”  alisema Mussa Kabalemesa.
Pia wafanyabiashara hao wameiomba serikali kuongeza eneo la kituo cha Makumbusho ili waweze kuhamia, kwani kwa sasa  eneo ni finyu.

0 comments:

Post a Comment