Friday, December 12, 2014

Mboga za majani ni nzuri kwa afya zetu Lakini wakati mwingine

 


Wakazi wa jiji la Dar es salaam wapo katika hatari ya kupatwa na magonjwa makubwa kama saratani, utasa, kupoteza uwezo wa kuona,kuharibu ubongo,maini na figo kutokana na matumizi ya mboga za majani zinazolimwa katika mabonde ya jiji hilo.


Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini humo,yakitokana na umuhimu wake kwa afya za watu na hali duni ya maisha inazozifanya familia nyingi kumudu gharama zake ikilinganishwa na vitoweo vingine.




 Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na kilimo kinachofanyika katika mbonde la mto Msimbazi na maeneo ya Kigogo-Sambusa,Ubungo,Gereji mchicha,Vingunguti na Tandale.


Katika Gazeti la NIPASHE limesema tayari matokeo ya tafiti kadhaa yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga za majani jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na kwenye makazi ya watu.








Pili wakazi wanaoishi pembezoni mwa bonde la Msimbazi na maeneo mengine yanayolimwa mboga hizo,wamebainika kutupa taka kama betri zilizoisha muda wa matumizi,masalia ya simu za mkononi,vipuri vya magari na majokofu mabovu.


Taka hizo zenye sumu zinatupwa kwenye mifereji ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga hivyo kuzidi kuhatarisha afya za walaji.



 Dk.Mwegoha alisema mboga zilizomwagiwa maji hayo zilibainika kuwa na sumu zilizokuwa na madini ya risasi,shaba na kromiamu ambazo zote zina madhara kwa binadamu.


Aliasema katika utafiti huo walibaini kuwa mboga hizo zinauzwa kwenye masoko ya Ilala, Kariakoo, Buguruni, Veterani,Tazara, Mwananyamala, Mnyamani, Kigogo, Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya jirani na wkaulima hao.
 

0 comments:

Post a Comment