Klabu ya Liverpool inajiamini kuwa inaweza kupokea kiasi cha pauni milioni 100 kutoka kwa Barcelona au Real Madrid kwa Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ameonekana kutupiwa sana macho na klabu hizo mbili kubwa kutoka Uhispania ambazo zinavutiwa sana na huduma yake.
Brendan Rodgers huenda akakubali kusikiliza ofa kwa klabu hizo lakini kwa kiasi ambacho kitavunja rekodi ya uhamisho wa Gareth Bale.
Arsenal wanajiandaa kumnunua Loic Remy na watakubali kutoa kiasi cha pauni milioni 10 ili kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo na klabu yake ya QPR.
Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anataka kupeleka ofa kwa kiungo wa Real Madrid,Sami Khedira mara baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika.
Meneja wa Arsenal,Arsene Wenger alikutana na wakala wa Mario Balotelli siku ya Jumapili nchini Brazil katika kujadili ofa ya pauni milioni 25 kwa mshambuliaji huyo wa AC Milan.
Tottenham wanamtupia macho winga wa klabu PSV ya Uholanzi,Memphis Depay na wameandaa kiasi cha pauni milioni 17 ili kuhakikisah aanatua White Hart Lane.
Mshambuliaji wa Manchester City,Alvaro Negredo anataka kuondoka klabuni hapo na kujiunga na Atletico Madrid majira haya ya joto.
Winga wa Southampton,Adam Lallana anataka kulazimisaha uhamisho wa kwenda Liverpool wakati atakaporejea nyumbani kutoka kwenye kampeni za Uingereza za kombe la dunia.
Everton inatazamia kumnyakua winga wa klabu ya Crystal Palace,Yannick Bolasie katika mipango ya kuimarisha kikosi cha Goodson Park.
Klabu ya Tottenham kutoka London inaandaa ofa ya kiasi cha pauni milioni 10 kwa mlinda mlango mahiri wa Newcastle United,Tim Krul.
Tottenham,Everton na Newcastle United zipo katika vita kali za kuwania saini ya mshambuliaji wa Ecuador,Enner Valencia.
Klabu ya Pachuca anayoichezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 imethibitisha kwamba tayari imeshapokea ofa kadhaa.
Kwa habari na tetesi nyingine za usajiri utazipata hapa....HABARI ZA MICHEZO.
0 comments:
Post a Comment