WAKATI abiria wa treni inayotoa usafiri katika Jiji la Dar es Salaam wakifikia milioni 1.4, Serikali imetenga Sh bilioni 2.92 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa njia mpya za reli jijini humo kutokana na huduma hiyo kukua na kupendwa na wananchi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ilisafirisha abiria 1,343,763 katika mwaka 2013 ikilinganishwa na abiria 230,009 waliosafirishwa katika mwaka 2012 kutoka Stesheni hadi Ubungo Maziwa.
Aidha, kwa upande wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), alisema abiria 1,460,506 walisafirishwa katika mwaka 2013 ikilinganishwa na abiria 148,524 waliosafirishwa katika mwaka 2012 kutoka Mwakanga hadi Kurasini.
Usafiri huo ni maarufu kwa jina la Treni ya Mwakyembe.
Akiwasilisha bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2014/15 bungeni Dodoma juzi usiku, Dk Mwakyembe alisema wizara inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma hiyo, ukiwamo mpango wa kuvutia sekta binafsi kuwekeza kwenye usafiri wa treni Jijini.
0 comments:
Post a Comment