• Gabriella Handbags

    Utazipata full na sandals zake 0654792227

  • Culture Tshirt

    Tunaprint na kuuza tshrt kwa bei rahisi 0655699674

  • Fashion watch

    ukihitaji saa za kijanja jumla na rejereje piga 0654792227

  • Reny Fashion

    Unaweza Tutembelea Duka lipo VIngunguti Stend ya Magari ya kwenda mijini pale kigorofani

  • Tshrt

Monday, March 16, 2015

ZIFAHAMU FAIDA ZA TANGAWIZI: NI DAWA INATIBU MAGONJWA LUKUKI ZIFAHAMU FAIDA ZA TANGAWIZI: NI DAWA INATIBU MAGONJWA LUKUKI

Tangawizi ni moja ya viungo vinavyotumika katika maandalizi ya vyakula tofauti tofauti pia mara nyingi katika nyama.
Wapishi wengi huamini kuwa nyama ikiwekwa tangawizi inalanika haraka na pia kuwa na ladha nzuri.
kwa asili tangwizi ina ladha kali kidogo ambayo watoto wadogo hawawezi kuivumilia,lakini mbali na hivyo kiungo hiki kinaweza kutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali mwilini ikwemo magonjwa ya ngozi!!
Tafiti zinasema Zao hili lina madini mbalimbali ikiwemo  :-                                                Magnesium, Potasium,Magnese, Vitamini B6 na Copper.
Ambayo hutumika katika mwili kupambana na magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu.



  •     Husaidia kutibu ugonjwa wa Gauti kwa kutibu sehemu zote za viungo zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
  •     Huasidia katika kusaga chakula, Hasa watu ambao wanapata taizo la haja kubwa. Tangawizi husaidia mfumo wa kusaga chakula tumboni.
  •     Husaidia tatizo la kuganda damu mwilini na kuondoa maumivu mwilini. Hapa ni katika msukumo wa damu mwilini.
  •     Tangawizi imetajwa kuwa ni dawa kwa shnikizo la damu.
  •     Nguvu za kiume,imeelezwa pia juice ya tangawizi husaidia kusukuma damu kwenye mishipa tofauti na pia ile ya via za kizazi.

Thursday, January 29, 2015

Jamani Mapenzi hayaaaaa

Kijana anaetuhumiwa kumchinja mpenzi wake sababu ya wivu wa mapenzi akiwa amepandishwa katika gari la Polisi akipelekwa kituoni huku akitokwa na damu shingoni baada ya kujaribu kujiua kwa kutumia kisu.Picha

 Mwili wa Msichana anaedaiwa kuchinjwa na mpenzi wake leo jioni maeneo ya Manzese Friends Corner ukitolewa katika eneo la tukio

Tuesday, December 16, 2014

Hii ndio yanga



Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe

Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni hapo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga imeshinda michezo minne msimu huu, lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya saba hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa haraka sana na mashabiki, wapenzi, wanachama na viongozi wa klabu yake kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya ufundishaji imekosa mvuto, lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba kimeshindwa kuvumilika.

COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa, ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi wachezaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye aliomba mwenyewe kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza katika kiwango cha kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya kwanza.

Jaja alifunga mara mbili dhidi ya Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha kufunga bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu. Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa wakipendezwa na kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa wengi. Maximo aliwanyima nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry Tegete, Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil waliposhindwa kufanya vizuri.

Kuwang’ang’ania wachezaji hao na kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts aliondolewa baada ya kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa viongozi kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.



Brandts ndiye mwalimu aliyeifanya Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank Domayo ( yuko Azam FC kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na wengineo lakini kwa Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘ wanasua-sua’. Yanga wamefanya uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.

Friday, December 12, 2014

Mboga za majani ni nzuri kwa afya zetu Lakini wakati mwingine

 


Wakazi wa jiji la Dar es salaam wapo katika hatari ya kupatwa na magonjwa makubwa kama saratani, utasa, kupoteza uwezo wa kuona,kuharibu ubongo,maini na figo kutokana na matumizi ya mboga za majani zinazolimwa katika mabonde ya jiji hilo.


Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini humo,yakitokana na umuhimu wake kwa afya za watu na hali duni ya maisha inazozifanya familia nyingi kumudu gharama zake ikilinganishwa na vitoweo vingine.




 Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na kilimo kinachofanyika katika mbonde la mto Msimbazi na maeneo ya Kigogo-Sambusa,Ubungo,Gereji mchicha,Vingunguti na Tandale.


Katika Gazeti la NIPASHE limesema tayari matokeo ya tafiti kadhaa yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga za majani jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na kwenye makazi ya watu.








Pili wakazi wanaoishi pembezoni mwa bonde la Msimbazi na maeneo mengine yanayolimwa mboga hizo,wamebainika kutupa taka kama betri zilizoisha muda wa matumizi,masalia ya simu za mkononi,vipuri vya magari na majokofu mabovu.


Taka hizo zenye sumu zinatupwa kwenye mifereji ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga hivyo kuzidi kuhatarisha afya za walaji.



 Dk.Mwegoha alisema mboga zilizomwagiwa maji hayo zilibainika kuwa na sumu zilizokuwa na madini ya risasi,shaba na kromiamu ambazo zote zina madhara kwa binadamu.


Aliasema katika utafiti huo walibaini kuwa mboga hizo zinauzwa kwenye masoko ya Ilala, Kariakoo, Buguruni, Veterani,Tazara, Mwananyamala, Mnyamani, Kigogo, Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya jirani na wkaulima hao.
 

Thursday, July 10, 2014

MTOTO MIAKA 3 AJISAIDIA HAJA KUBWA KWA NJIA YA MDOMO













MASKINI Mungu wangu! Ndiyo maneno aliyoanza nayo kusema mama mzazi wa mtoto Salome Abdallah Said (3), kutokana na mwanaye huyo afya yake kuzidi kubadilika kufuatia kuumwa mara kwa mara licha ya kufanyiwa upasuaji mara mbili.



Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama wa mtoto huyo Veronica Laurent, mkazi wa Bunju B, jijini Dar es Salaam alisema kwamba mwanaye kwa sasa hali yake siyo nzuri kwa vile amekuwa akijisaidia haja kubwa kupitia mdomoni kama hapo awali, hali hiyo anasema ameambiwa na madaktari inasababishwa na utumbo wake wa haja kubwa kujikunja.











HISTORIA YA MTOTO
Veronica anaeleza: “Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu, tangu nimzae katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar, aligundulika ana matatizo ya kutojisaidia haja kubwa kama kawaida ilibidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

“Nilimfikisha Muhimbili akiwa katika hali mbaya akawa anajisaidia haja kubwa kupitia mdomoni, hata hivyo, nikaambiwa tumpeleke Hospitali ya Agha Khan kwa vipimo zaidi, huko akagundulika kuwa utumbo wa haja kubwa umejikunja.”



AFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI
Katika maelezo yake mama huyo alisema kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji kwa mara ya kwanza tumboni na kuwekwa tundu ambalo alikuwa akilitumia kutolea haja kubwa, baadaye akafanyiwa tena upasuaji kwa mara ya pili chini ya tumbo na kuwekewa utumbo bandia lakini hata hivyo, ulikuwa mwembamba hivyo ukawa haufanyi kazi vizuri.







UTUMBO WA BANDIA
“Tulipotoka Muhimbili na kurejea nyumbani haikuchukua siku nyingi hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya, akawa analia kila mara nikaamua kurudi Muhimbili.

“Madaktari baada ya uchunguzi wakasema utumbo wa bandia aliowekewa ulikuwa mdogo na mwembamba hivyo ulishindwa kufanya kazi pia utumbo ulikuwa umejikunja.
“Niliambiwa zinahitajika shilingi laki tisa ili afanyiwe matibabu ambapo nimeshindwa kuzipata, bora awamu ya kwanza alijitokeza mdhamini akatoa shilingi laki tisa. Nawaaomba Watanzania wenzangu wamsaidie mwanangu ili kumnusuru na kifo, maana madaktari wamesema bila kufanyiwa hivyo anaweza kupoteza maisha,” alisema mama huyo.

Akifafanua zaidi alisema: “Wakati fulani ili apitishe haja kubwa katika njia ya kawaida inabidi ninunue dawa ya kulainisha kinyesi kwani bila kufanya hivyo ni lazima ajisaidie kwa kupitia mdomoni.”

BABA YAKE ATOROKA
“Kwa sasa mtoto halali kutokana na kulia kutokana na maumivu makali, baba yake baada ya kuona tatizo la huyu mwanangu alitoweka na kuzima simu, hapatikani. Mimi nashindwa kufanya kazi yoyote.
Nawaomba Watanzania mnisaidie kupitia namba yangu ya simu 0712 004 677 au 0767 026 551,” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na machozi.






Thursday, July 3, 2014

MTOTO AFUNGIWA KWENYE BANDA LA MBUZI KWA MIAKA 10


Nairobi. Juni 21 ilikuwa ni siku ya kawaida kwa Mama Nancy mkazi wa Narok nchini Kenya, lakini ilifichua siri nzito ya mtoto aliyefichwa kwa miaka kumi katika banda la mbuzi.
Akiwa katika shughuli zake za nyumbani, mara akatokea mtoto mdogo wa jirani yake aitwaye Jane.       
Binti huyo akaanza kucheza na wenzake kwa dakika kadhaa na mara akaacha michezo na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani kwao.
Wenzake wakamuuliza “mbona unakimbia wakati bado tunacheza”. Akajibu, “nakwenda kwenye banda la mifugo kumpa chakula Ben. Muda umekimbia na hakuna mtu nyumbani”.
Kwa kauli hiyo, mwanamke huyo alitaka kujua iwapo Ben anaishi kwenye nyumba ya jirani yake kwani ni miaka 10 imepita tangu amtie machoni.
“Ben yupo na anaishi kwenye banda la mifugo. Huwa anahudumiwa na mama, lakini kwa sasa mama hayupo na baba amekwenda kazini. Mimi nina jukumu la kumpa chakula,” alijibu Jane.
Mama huyo akapata shauku ya kumtembelea mtoto huyo kuona kinachoendelea kwa jirani zake, Lo! anachokiona haamini macho yake; Mtoto Ben amefungwa kwa kamba kwenye kigodoro chembamba akiwa hajiwezi kwa njaa.
Hivyo ndivyo alivyoibuliwa mtoto Ben baada ya kukaa katika banda la mbuzi kwa muda wa miaka 10 bila majirani kufahamu.
Ben, ambaye kwa sasa ana miaka   miaka 14 alizaliwa akiwa kiziwi, bubu   na ulemavu. Aibu ya kuzaa mtoto kama huyo ndiyo ilifanya wazazi wake wamfungie kwenye zizi la wanyama kwa muda wa miaka 10 na wakihakikisha  hakuna jirani wala ndugu wa karibu anayefahamu juu ya tukio hilo.
Historia ya mtoto huyo
Kwa mujibu wa baba mlezi Mr Jeremiah Mbusia,  ambaye ni askari katika Wizara ya Mali Asili, Narok Kenya, mtoto  huyo siyo wake wa kuzaa bali alifika katika nyumba hiyo miaka 12 iliyopita akiwa na mama yake wakati huo mtoto huyo alikuwa na miaka minne.
Alilelewa katika nyumba hiyo kwa miaka miwili na ndipo wazazi wake, yaani baba yake wa kambo na mama yake mzazi wakaamua kumuweka katika kibanda kidogo nje ya nyumba yao  na hutumiwa kama zizi la mbuzi na kondoo.

Wednesday, July 2, 2014

DIAMOND PLATNUM NDANI YA BET RED CARPET




Diamond Platnumz akipita kwenye Red Carpet ya BET mbele ya mapaparazi zaidi ya 200. Mwanamuziki huyu alionekana kuwavutia watu wengi na suti yake iliyokuwa imemkaa kisawasawa ambayo Waingereza wanasema "Well Tailored Suit" By Designer Sheria Ngowi .



Mapaparazi zaidi ya 200 walichukua every step and moments za Red Carpet wakati Diamond akipita.…

Diamond akiwa anaongea na Neyo kwenye Red carpet

     
                                    Akiwa kwenye pozi tata lililowavutia mapaparazi

                                                    Akiwa anahojiwa na factory 78 ya UK...

                                      Hapa akihojiwa na karrueche Tran kwenye Red capert
                                                 (karrueche ni girlfriend wa Chris brown)

                                                 akiwa na Nelly kwenye Red Carpet

Kwa hakika anastahili pongezi anaitambulisha vizuri nchi yetu hata kama alikosa Tuzo.